UTAMU WA IMANI

UTAMU WA IMANI

Share

kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu IMANI, HASWA IMANI YA AGANO JIPYA

01/09/2026
01/09/2026

Ufalme wa Mungu ni utawala wa Mungu katika maisha ya mwanadamu, ambapo Mungu ndiye mwenye mamlaka, na watu huishi kwa haki, upendo, amani na utiifu kwa mapenzi yake.
📖 “Ufalme wa Mungu umo ndani yenu.” — Luka 17:21

01/09/2026

Mwezi mpya wa September Anza mwezi kwa KUMSHUKURU MUNGU

27/08/2026

Mathayo 28:12

Wakakusanyika pamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi.”

UJUMBE WA LEO

Baada ya kufanya shauri la kuficha ukweli, walitumia fedha nyingi kuwashawishi askari. Hapa tunaona kwamba fedha inaweza kuwa chombo cha kufanya jambo jema au chombo cha kununua jambo baya.

Biblia haifundishi kwamba fedha yenyewe ni mbaya. Tatizo ni nafasi tunayoipa fedha katika maisha yetu. Kupenda fedha ni shina moja la kila namna ya mabaya (1 Timotheo 6:10). Fedha inapovuka mipaka yake, inaweza kuanza kuwa bwana badala ya kuwa chombo.

Tunaweza kulinganisha jambo hili na Edeni. Mungu aliweka miti mingi mbele ya Adamu na Hawa, lakini kulikuwa na mti mmoja ambao aliweka mpaka juu yake: “Msile matunda yake” (Mwanzo 2:16–17). Mungu hakuwanyima kila kitu, aliwafundisha baraka pia zina mipaka.

Leo hatuko Edeni, lakini tunaishi katika dunia ambayo fedha imekuwa k**a “tunda la mti wa katikati.” Fedha iko katikati ya maamuzi mengi ya maisha mfano elimu, biashara, siasa, ajira, huduma, mahusiano, mamlaka na hata dini. Fedha yenyewe si dhambi lakini inapowekwa katikati ya kila kitu, inaweza kuwa jaribu linalomfanya mtu avunje mipaka aliyowekewa na Mungu.

Shetani katika Edeni hakumshawishi mwanadamu kwa kumwambia moja kwa moja, “Mtii mimi.” Alianza kwa kumfanya mwanadamu atamani kile Mungu alikuwa ameweka mpaka. Leo jaribu linaweza kuja kwa namna nyingine: “Pata fedha zaidi; usijali imepatikana vipi.” Hapo ndipo fedha inaweza kuwa mtego.

Kwa hiyo, tatizo si kuwa na fedha nyingi, tatizo ni pale fedha inapokuwa na mamlaka kubwa kwako kuliko inavyostahili. Mtu anaweza kuwa na fedha nyingi kamtumikia Mungu lakini mwingine ana fedha kidogo akawa mtumwa wa fedha.

KANUNI ZA MIPAKA YA FEDHA

K**a Mungu alivyoweka mpaka kwenye tunda la Edeni, Mkristo anahitaji kuweka mipaka ya fedha.

Mpaka wa kwanza ni chanzo:
“Nitapataje fedha?”
Si kila fedha inayoweza kupatikana inapaswa kupatikana. Fedha ya rushwa, udanganyifu, wizi au unyonyaji haibadiliki kuwa halali kwa sababu tu imeleta faida.

Mpaka wa pili ni kiasi:
“Nahitaji kiasi gani?”
Tamaa haina mwisho. Mtu akisema, “Nikifikisha hiki nitatosheka,” anaweza kufika hapo na kuanza kutaka kingine. Hivyo tunahitaji kujifunza kuridhika na kuweka mipaka ya tamaa.

Mpaka wa tatu ni matumizi:
“Nitumie fedha yangu kwa nini?”
Si kila kitu tunachoweza kununua tunapaswa kununua. Fedha inahitaji bajeti, vipaumbele na nidhamu. Mungu hakutupa fedha ili kila tamaa itawale matumizi yetu.

Mpaka wa nne ni mamlaka:
“Fedha inaweza kunifanya nifanye nini?”
Hapa ndipo Mathayo 28 inakuwa muhimu. Viongozi walikuwa tayari kutumia fedha nyingi ili kubadilisha ukweli. Fedha inapoweza kununua dhamiri yako, tayari imevuka mpaka.

Mpaka wa tano ni mahusiano:
Usitumie fedha kununua upendo, uaminifu, urafiki au heshima. Mtu anayekupenda kwa sababu ya fedha anaweza kukuacha fedha zinapoisha.

Mpaka wa sita ni Mungu:
Fedha haiwezi kuwa zaidi ya Mungu. Yesu alisema, “Hamuwezi kumtumikia Mungu na mali” (Mathayo 6:24). Mali ni chombo; Mungu ndiye Bwana.

Kwa hiyo, mpendwa jifunze kusema: “Nina fedha, lakini fedha hainimiliki. Ninaweza kuitumia, lakini siwezi kuiabudu. Naweza kuitafuta, lakini siwezi kuivunja mipaka ya Mungu kwa ajili yake.”

WAZO KUU LA LEO

Fedha ni baraka inapokuwa chombo mikononi mwako, lakini ni mtego wa mauti inapokuwa bwana wa moyo wako.

MASWALI YA KUJIULIZA

1. Je, fedha imenisaidia kumtumikia Mungu au imeanza kunitawala?

2. Ni mpaka gani wa fedha ambao nimeuweka katika maisha yangu?

MAOMBI

Bwana Mungu wangu, nakushukuru kwa uwezo wa kufanya kazi na kupata mali. Nifundishe kuitumia fedha k**a chombo na si kuifanya kuwa bwana wa maisha yangu. Nipe hekima ya kuweka mipaka katika kupata, kuhifadhi na kutumia fedha. Nilinde dhidi ya tamaa, rushwa na udanganyifu. Usiruhusu fedha inunue dhamiri yangu, ibadilishe imani yangu au kunifanya nivunje kanuni zako. Nisaidie kuwa mwaminifu katika mali uliyonikabidhi. Katika jina la Yesu Kristo. Amina.

BARAKA ZA LEO

Mungu akubariki kwa fedha inayotokana na kazi yenye haki. Akupe hekima ya kuitawala kabla haijaanza kukutawala. Akulinde dhidi ya tamaa, rushwa na mitego ya utajiri. Uwe na fedha bila kuwa mtumwa wa fedha, uwe na mali bila kuipoteza roho yako, na utumie kila ulichopewa kwa utukufu wa Mungu na baraka kwa wengine. Amina.

đź“… 27.08.2026
UJUMBE KUTOKA KWA MTUMISHI WA MUNGU

✍️ Mchg. Jasson Joas Kahembe
⛪

26/08/2026

_“Njia za mwenye haki” ni njia ya maisha inayompendeza Mungu—kuishi kwa imani, utii, unyenyekevu na kutenda yaliyo mema mbele zake.

đź“– Maana ya njia za- mwenye haki
Ni njia inayoongozwa na Mungu
Mwenye haki hamtegemei Mungu kwa maneno tu, bali humruhusu Mungu aongoze maamuzi na hatua zake.

👉Mithali 3:5–6: “Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote… naye atayanyosha mapito yako.”
Ni njia ya uadilifu na kweli
Mwenye haki hachagui uongo kwa sababu ya faida. Anasimama katika kweli hata inapokuwa ngumu.

👉Zaburi 15:1–2 inaeleza mtu anayekaa mbele za Mungu kuwa ni yule aendaye kwa ukamilifu na kusema kweli moyoni mwake.
Ni njia ya kumcha Mungu
Kumcha Mungu si kumuogopa tu, bali ni kumheshimu na kuchukia uovu.

👉Mithali 8:13: “Kumcha Bwana ni kuchukia uovu.”
Ni njia yenye majaribu lakini Mungu huwa pamoja naye
Kuwa mwenye haki hakumaanishi kutokutana na matatizo. Biblia inasema:

👉Zaburi 34:19: “Mateso ya mwenye haki ni mengi, lakini Bwana humponya nayo yote.”
Ni njia inayozidi kuwa angavu

👉Mithali 4:18: “Bali njia ya wenye haki ni k**a nuru ing’aayo, ikizidi kung’aa hata mchana mkamilifu.”
Hii inatufundisha kwamba Mungu humwongoza mwenye haki hatua kwa hatua kuelekea kwenye nuru zaidi.

Mwisho wake ni uzima
Mwenye haki anaweza kupitia changamoto duniani, lakini njia yake inaelekea kwenye uzima na uwepo wa Mungu.

Zaburi 1:6: “Kwa kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki; bali njia ya wasio haki itapotea.”

🔥 Ujumbe muhimu
Njia ya mwenye haki si njia isiyo na changamoto; ni njia ambayo Mungu yupo ndani yake. Wakati mwingine unaweza kuona k**a umechelewa, unapitia majaribu au mambo hayaendi k**a ulivyotarajia, lakini endelea kumtumaini Mungu. Usiachane na njia ya haki kwa sababu ya shida ya muda mfupi.

26/08/2026

Msamaha katika agano la kale haukuwa na nguvu ndo maana Yesu akaja

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Manyara?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Website

Address

Manyara
Manyara