Iringa Recovery Community - IRC
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Iringa Recovery Community - IRC, Non-Governmental Organization (NGO), Iringa.
A community-based organization supporting individuals and families affected by addiction through recovery services, awareness, and empowerment.
π Based in Iringa, Tanzania
17/08/2026
13/08/2026
Tarehe 07 Agosti 2026, IRC ilipata heshima ya kuwapokea wanachama wa Club ya Anti-Drug kutoka Ilula, waliotutembelea kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu katika mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya.
Katika ziara hiyo, wageni walipata fursa ya kujifunza kupitia uzoefu wa clients katika recovery, hususan namna ya kupunguza uwezekano wa relapse na umuhimu wa kuwawezesha watu katika recovery kujenga maisha yenye mwelekeo chanya.
Tulijadili pia nafasi ya life skills na ujuzi wa vitendo, ikiwemo ufundi na shughuli nyingine za uzalishaji, katika kumsaidia mtu kujitegemea, kujenga kujiamini, kutumia muda vizuri na kuimarisha safari yake ya recovery.
IRC tunaamini kuwa recovery si kuacha matumizi ya dawa za kulevya pekee; ni kujenga upya maisha. Ndiyo maana tunaendelea kuwekeza katika elimu, afya ya akili, life skills, ushirikiano wa jamii na kuwawezesha individuals kujenga maisha yenye afya na matumaini. π±
Tunawashukuru Club ya Anti-Drug Ilula kwa kututembelea na kwa kuendelea kuwa sehemu ya harakati hii.
Together, we prevent. Together, we recover. Together, we rebuild lives. π
MentalHealth YouthEmpowerment CommunityRecovery AntiDrug RecoveryJourney
07/07/2026
K**a Wanyama wakitumia Dawa za Kulevya huwavuruga na kuwawafanya kuwa wenye fujo na vurugu, vipi wewe? π
Epuka matumizi ya Dawa za Kulevya, Ni hatari sana.
Credits: The Safari Podcast
Katika kipindi cha maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoanza rasmi mwezi Aprili na kuhitimishwa tarehe 16 Juni 2026, Iringa Recovery Community (IRC) ilipata nafasi kubwa ya kushiriki kikamilifu kupitia Mwanasaikolojia John John, ambaye aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa K**ati ya Maandalizi ya maadhimisho hayo ndani ya Manispaa ya Iringa.
Kupitia nafasi hiyo, Mr. John John Psychologist JOHN JOHN ameongoza shughuli mbalimbali za utoaji elimu katika maeneo tofauti ya Manispaa ya Iringa, akigusia mada muhimu zenye lengo la kumlinda na kumjenga mtoto wa Afrika. Mada hizo zimehusisha ukatili dhidi ya watoto, afya ya akili, kujitambua, pamoja na masuala mengine muhimu yanayolenga kupinga ukatili wa aina yoyote dhidi ya mtoto.
Maadhimisho haya yamefanikiwa kufanyika kwa ushirikiano mkubwa kati ya Serikali, wadau mbalimbali wa maendeleo, na taasisi zinazofanya kazi za kijamii ndani ya Manispaa ya Iringa. Kwa niaba ya wadau wote, Mr. John John alipata nafasi ya kutoa hotuba yenye ujumbe mzito na wa kugusa maeneo muhimu katika harakati za kutetea haki, usalama, na ustawi wa mtoto wa Kiafrika.
K**a taasisi, IRC itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kupinga ukatili dhidi ya watoto na jinsia, kusimamia haki za binadamu, na kutoa elimu pamoja na msaada wa kisaikolojia na afya ya akili kwa jamii. Tunaamini kuwa kupitia ushirikiano na Serikali pamoja na wadau wengine, tunaweza kuendelea kuikomboa jamii yetu kiakili, kijamii na kiuchumi.
Endelea kutufuatilia kupitia kurasa zetu kwa taarifa zaidi kuhusu kazi tunazoendelea kufanya katika kuijenga jamii salama, yenye afya na matumaini kwa watoto, vijana na familia kwa ujumla πβ¨
NB: Mtuwie radhi kwa uhafifu wa video hii, ila kwa umuhimu wake imetulazimu kuitumia.
Maneno ya mch Hananja katika uzinduzi wa Filamu ya Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya.
Pongezi kwa Drug Control and Enforcement Authority
Youth Empowerment & Psychotherapy Aid Organization
Drug Abuse Prevention Org (DAPO) Muungano Recovery Community TZ Gift Ofh Vision of Hope Initiative
Neno kutoka kwa Brother ChidBeenz
cc: .inc
Click here to claim your Sponsored Listing.