Arusha Technical College

Arusha Technical College

Share

The College is located at the Central Business District of the Arusha City which is the Northern Tanzania’s centre of agriculture, commerce, trade and tourism.

Arusha Technical College is a center of excellence that provides a national and international high-level human resource through exemplary competence based Technical Education and training in Tanzania. The institution which has become the Arusha Technical College (ATC), was established in 1978 jointly by the Governments of the United Republic of Tanzania and Germany, under the name of the Technical

Photos from Arusha Technical College's post 01/06/2026

ATC C na UNDP Wasaini Makubaliano ya Kuimarisha Fursa kwa Vijana

Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kimkakati utakaowezesha kufunguliwa kwa fursa zaidi kwa vijana kupitia maendeleo ya ujuzi, ubunifu, ujasiriamali na ajira.

Hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo ilifanyika tarehe 29 Mei 2026 katika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Mkuu wa Chuo cha ATC, Prof. Musa N. Chacha.

Makubaliano hayo yanalenga kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za elimu ya juu na wadau wa maendeleo ili kuzalisha wahitimu wenye ujuzi na uwezo unaokidhi mahitaji ya soko la ajira na maendeleo ya uchumi wa kisasa.

Kupitia ushirikiano huu, ATC na UNDP zitashirikiana katika kuendeleza ubunifu, ujasiriamali, kujenga uwezo wa vijana na kuimarisha fursa za maendeleo, hatua itakayochangia ustawi wa kijamii na kiuchumi pamoja na kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika maendeleo endelevu ya Tanzania

27/05/2026
19/05/2026

Appointments

Photos from Arusha Technical College's post 15/05/2026

𝗗𝗸𝘁. 𝗡𝗼𝗲𝗹 𝗠𝗯𝗼𝗻𝗱𝗲 𝗔𝗶𝗽𝗼𝗻𝗴𝗲𝘇𝗮 𝗦𝗢𝗔𝗧𝗘𝗖𝗢 𝗸𝘄𝗮 𝘂𝗯𝘂𝗻𝗶𝗳𝘂 𝗺𝗽𝘆𝗮

•Azindua Programu ya Akili ‘SOATECO AI’

𝘔𝘸𝘦𝘯𝘺𝘦𝘬𝘪𝘵𝘪 𝘸𝘢 𝘉𝘰𝘥𝘪 𝘺𝘢 𝘜𝘵𝘢𝘸𝘢𝘭𝘢 𝘺𝘢 𝘊𝘩𝘶𝘰 𝘤𝘩𝘢 𝘜𝘧𝘶𝘯𝘥𝘪 𝘈𝘳𝘶𝘴𝘩𝘢, 𝘋𝘬𝘵. 𝘕𝘰𝘦𝘭 𝘔𝘣𝘰𝘯𝘥𝘦, 𝘢𝘮𝘦𝘪𝘱𝘰𝘯𝘨𝘦𝘻𝘢 𝘚𝘦𝘳𝘪𝘬𝘢𝘭𝘪 𝘺𝘢 𝘞𝘢𝘯𝘢𝘧𝘶𝘯𝘻𝘪 𝘺𝘢 𝘚𝘖𝘈𝘛𝘌𝘊𝘖 𝘬𝘸𝘢 𝘬𝘶𝘻𝘪𝘯𝘥𝘶𝘢 𝘱𝘳𝘰𝘨𝘳𝘢𝘮𝘶 𝘺𝘢 𝘈𝘬𝘪𝘭𝘪 𝘔𝘯𝘦𝘮𝘣𝘢 𝘪𝘯𝘢𝘺𝘰𝘫𝘶𝘭𝘪𝘬𝘢𝘯𝘢 𝘬𝘢𝘮𝘢 𝘚𝘖𝘈𝘛𝘌𝘊 𝘈𝘐,

𝘮𝘧𝘶𝘮𝘰 𝘶𝘵𝘢𝘬𝘢𝘰𝘳𝘢𝘩𝘪𝘴𝘪𝘴𝘩𝘢 𝘶𝘱𝘢𝘵𝘪𝘬𝘢𝘯𝘢𝘫𝘪 𝘸𝘢 𝘵𝘢𝘢𝘳𝘪𝘧𝘢 𝘮𝘣𝘢𝘭𝘪𝘮𝘣𝘢𝘭𝘪 𝘻𝘪𝘯𝘢𝘻𝘰𝘩𝘶𝘴𝘪𝘢𝘯𝘢 𝘯𝘢 𝘤𝘩𝘶𝘰.𝘈𝘬𝘪𝘻𝘶𝘯𝘨𝘶𝘮𝘻𝘢 𝘬𝘢𝘵𝘪𝘬𝘢 𝘩𝘢𝘧𝘭𝘢 𝘩𝘪𝘺𝘰, 𝘋𝘬𝘵. 𝘔𝘣𝘰𝘯𝘥𝘦 𝘢𝘮𝘦𝘴𝘦𝘮𝘢 𝘶𝘻𝘪𝘯𝘥𝘶𝘻𝘪 𝘸𝘢 𝘮𝘧𝘶𝘮𝘰 𝘩𝘶𝘰 𝘯𝘪 𝘩𝘢𝘵𝘶𝘢 𝘮𝘶𝘩𝘪𝘮𝘶 𝘺𝘢 𝘮𝘢𝘦𝘯𝘥𝘦𝘭𝘦𝘰 𝘺𝘢 𝘬𝘪𝘥𝘪𝘫𝘪𝘵𝘢𝘭𝘪 𝘯𝘥𝘢𝘯𝘪 𝘺𝘢 𝘵𝘢𝘢𝘴𝘪𝘴𝘪 𝘻𝘢 𝘦𝘭𝘪𝘮𝘶, 𝘬𝘸𝘢𝘯𝘪 𝘶𝘵𝘢𝘴𝘢𝘪𝘥𝘪𝘢 𝘸𝘢𝘯𝘢𝘧𝘶𝘯𝘻𝘪 𝘬𝘶𝘱𝘢𝘵𝘢 𝘵𝘢𝘢𝘳𝘪𝘧𝘢 𝘬𝘸𝘢 𝘩𝘢𝘳𝘢𝘬𝘢 𝘯𝘢 𝘬𝘸𝘢 𝘶𝘳𝘢𝘩𝘪𝘴𝘪 𝘻𝘢𝘪𝘥𝘪 𝘣𝘪𝘭𝘢 𝘷𝘪𝘬𝘸𝘢𝘻𝘰 𝘷𝘺𝘢 𝘮𝘶𝘥𝘢 𝘢𝘶 𝘮𝘢𝘩𝘢𝘭𝘪.
𝘈𝘪𝘥𝘩𝘢, 𝘢𝘮𝘦𝘸𝘢𝘵𝘢𝘬𝘢 𝘷𝘪𝘰𝘯𝘨𝘰𝘻𝘪 𝘸𝘢 𝘴𝘦𝘳𝘪𝘬𝘢𝘭𝘪 𝘺𝘢 𝘸𝘢𝘯𝘢𝘧𝘶𝘯𝘻𝘪 𝘬𝘶𝘩𝘢𝘬𝘪𝘬𝘪𝘴𝘩𝘢 𝘸𝘢𝘯𝘢𝘬𝘶𝘸𝘢 𝘯𝘢 𝘮𝘱𝘢𝘯𝘨𝘰 𝘸𝘢 𝘮𝘢𝘣𝘢𝘥𝘪𝘭𝘪𝘬𝘰 𝘺𝘢 𝘶𝘰𝘯𝘨𝘰𝘻𝘪 ‘𝘴𝘶𝘤𝘤𝘦𝘴𝘴𝘪𝘰𝘯 𝘱𝘭𝘢𝘯’ 𝘪𝘭𝘪 𝘷𝘪𝘰𝘯𝘨𝘰𝘻𝘪 𝘚𝘦𝘳𝘪𝘬𝘢𝘭𝘪 𝘺𝘢 𝘞𝘢𝘯𝘢𝘧𝘶𝘯𝘻𝘪 𝘸𝘢𝘵𝘢𝘬𝘢𝘰𝘬𝘶𝘫𝘢 𝘣𝘢𝘢𝘥𝘢𝘺𝘦 𝘸𝘢𝘸𝘦𝘻𝘦 𝘬𝘶𝘦𝘯𝘥𝘦𝘭𝘦𝘻𝘢 𝘮𝘢𝘧𝘢𝘯𝘪𝘬𝘪𝘰 𝘯𝘢 𝘮𝘪𝘳𝘢𝘥𝘪 𝘪𝘭𝘪𝘺𝘰𝘢𝘯𝘻𝘪𝘴𝘩𝘸𝘢 𝘯𝘢 𝘸𝘢𝘭𝘪𝘰𝘵𝘢𝘯𝘨𝘶𝘭𝘪𝘢.𝘗𝘪𝘢 𝘢𝘮𝘦𝘴𝘪𝘴𝘪𝘵𝘪𝘻𝘢 𝘶𝘮𝘶𝘩𝘪𝘮𝘶 𝘸𝘢 𝘬𝘶𝘭𝘪𝘯𝘥𝘢 𝘣𝘶𝘯𝘪𝘧𝘶 𝘩𝘪𝘺𝘰 𝘬𝘸𝘢 𝘬𝘶𝘪𝘴𝘢𝘫𝘪𝘭𝘪 𝘳𝘢𝘴𝘮𝘪 𝘬𝘢𝘮𝘢 𝘩𝘢𝘬𝘪 𝘮𝘪𝘭𝘪𝘬𝘪 ‘𝘐𝘯𝘵𝘦𝘭𝘭𝘦𝘤𝘵𝘶𝘢𝘭 𝘗𝘳𝘰𝘱𝘦𝘳𝘵𝘺’, 𝘪𝘭𝘪 𝘬𝘶𝘩𝘢𝘬𝘪𝘬𝘪𝘴𝘩𝘢 𝘪𝘯𝘢𝘭𝘪𝘯𝘥𝘸𝘢 𝘬𝘪𝘴𝘩𝘦𝘳𝘪𝘢 𝘯𝘢 𝘬𝘶𝘻𝘶𝘪𝘢 𝘸𝘢𝘵𝘶 𝘸𝘦𝘯𝘨𝘪𝘯𝘦 𝘬𝘶𝘪𝘵𝘶𝘮𝘪𝘢 𝘣𝘪𝘭𝘢 𝘶𝘵𝘢𝘳𝘢𝘵𝘪𝘣𝘶.
𝘝𝘪𝘭𝘦𝘷𝘪𝘭𝘦, 𝘢𝘮𝘦𝘸𝘢𝘩𝘪𝘮𝘪𝘻𝘢 𝘸𝘢𝘯𝘢𝘧𝘶𝘯𝘻𝘪 𝘬𝘶𝘦𝘯𝘥𝘦𝘭𝘦𝘢 𝘬𝘶𝘣𝘶𝘯𝘪 𝘵𝘦𝘬𝘯𝘰𝘭𝘰𝘫𝘪𝘢 𝘯𝘢 𝘣𝘶𝘯𝘪𝘧𝘶 𝘮𝘣𝘢𝘭𝘪𝘮𝘣𝘢𝘭𝘪 𝘻𝘪𝘵𝘢𝘬𝘢𝘻𝘰𝘸𝘢𝘯𝘶𝘧𝘢𝘪𝘴𝘩𝘢 𝘸𝘢𝘰 𝘯𝘢 𝘫𝘢𝘮𝘪𝘪 𝘬𝘸𝘢 𝘶𝘫𝘶𝘮𝘭𝘢, 𝘬𝘸𝘢 𝘭𝘦𝘯𝘨𝘰 𝘭𝘢 𝘬𝘶𝘴𝘢𝘪𝘥𝘪𝘢 𝘬𝘶𝘵𝘢𝘵𝘶𝘢 𝘤𝘩𝘢𝘯𝘨𝘢𝘮𝘰𝘵𝘰 𝘮𝘣𝘢𝘭𝘪𝘮𝘣𝘢𝘭𝘪.

𝐌𝐭𝐚𝐦𝐛𝐨 𝐰𝐚 𝐊𝐮𝐟𝐮𝐚 𝐔𝐦𝐞𝐦𝐞 𝐰𝐚 𝐊𝐢𝐤𝐮𝐥𝐞𝐭𝐰𝐚 𝐊𝐮𝐤𝐚𝐦𝐢𝐥𝐢𝐤𝐚 𝐍𝐨𝐯𝐞𝐦𝐛𝐚 𝟐𝟎𝟐𝟔. 15/05/2026

https://youtu.be/DNnH2JjsCWs

𝐌𝐭𝐚𝐦𝐛𝐨 𝐰𝐚 𝐊𝐮𝐟𝐮𝐚 𝐔𝐦𝐞𝐦𝐞 𝐰𝐚 𝐊𝐢𝐤𝐮𝐥𝐞𝐭𝐰𝐚 𝐊𝐮𝐤𝐚𝐦𝐢𝐥𝐢𝐤𝐚 𝐍𝐨𝐯𝐞𝐦𝐛𝐚 𝟐𝟎𝟐𝟔. 𝘒𝘪𝘵𝘶𝘰 𝘤𝘩𝘢 𝘒𝘪𝘬𝘢𝘯𝘥𝘢 𝘤𝘩𝘢 𝘜𝘮𝘢𝘩𝘪𝘳𝘪 𝘤𝘩𝘢 𝘔𝘢𝘧𝘶𝘯𝘻𝘰 𝘺𝘢 𝘕𝘪𝘴𝘩𝘢𝘵𝘪 𝘑𝘢𝘥𝘪𝘥𝘪𝘧𝘶 𝘬𝘢𝘵𝘪𝘬𝘢 𝘊𝘩𝘶𝘰 𝘤𝘩𝘢 𝘜𝘧𝘶𝘯𝘥𝘪 ?....

Photos from Arusha Technical College's post 15/05/2026

𝐌𝐭𝐚𝐦𝐛𝐨 𝐰𝐚 𝐊𝐮𝐟𝐮𝐚 𝐔𝐦𝐞𝐦𝐞 𝐰𝐚 𝐊𝐢𝐤𝐮𝐥𝐞𝐭𝐰𝐚 𝐊𝐮𝐤𝐚𝐦𝐢𝐥𝐢𝐤𝐚 𝐍𝐨𝐯𝐞𝐦𝐛𝐚 𝟐𝟎𝟐𝟔.

📍𝐾𝑢𝑧𝑖𝑏𝑎 𝑃𝑒𝑛𝑔𝑜 𝑙𝑎 𝑈𝑚𝑒𝑚𝑒 𝐾𝑎𝑛𝑑𝑎 𝑦𝑎 𝐾𝑎𝑠𝑘𝑎𝑧𝑖𝑛𝑖 𝑛𝑎 𝐾𝑢𝑜𝑘𝑜𝑎 𝐹𝑒𝑑ℎ𝑎 𝑧𝑎 𝐾𝑖𝑔𝑒𝑛𝑖.

Na ATC

𝘒𝘪𝘵𝘶𝘰 𝘤𝘩𝘢 𝘒𝘪𝘬𝘢𝘯𝘥𝘢 𝘤𝘩𝘢 𝘜𝘮𝘢𝘩𝘪𝘳𝘪 𝘤𝘩𝘢 𝘔𝘢𝘧𝘶𝘯𝘻𝘰 𝘺𝘢 𝘕𝘪𝘴𝘩𝘢𝘵𝘪 𝘑𝘢𝘥𝘪𝘥𝘪𝘧𝘶 𝘬𝘢𝘵𝘪𝘬𝘢 𝘊𝘩𝘶𝘰 𝘤𝘩𝘢 𝘜𝘧𝘶𝘯𝘥𝘪 𝘈𝘳𝘶𝘴𝘩𝘢 (𝘈𝘛𝘊) 𝘬𝘢𝘮𝘱𝘢𝘴𝘪 𝘺𝘢 𝘒𝘪𝘬𝘶𝘭𝘦𝘵𝘸𝘢 𝘪𝘭𝘪𝘤𝘩𝘰𝘱𝘰 𝘞𝘪𝘭𝘢𝘺𝘢 𝘏𝘢𝘪, 𝘔𝘬𝘰𝘢 𝘸𝘢 𝘒𝘪𝘭𝘪𝘮𝘢𝘯𝘫𝘢𝘳𝘰 𝘬𝘪𝘯𝘢𝘵𝘢𝘳𝘢𝘫𝘪𝘸𝘢 𝘬𝘶𝘻𝘢𝘭𝘪𝘴𝘩𝘢 𝘮𝘦𝘨𝘢𝘸𝘢𝘵𝘪 1.65 𝘻𝘢 𝘶𝘮𝘦𝘮𝘦 𝘻𝘪𝘵𝘢𝘬𝘢𝘻𝘰𝘴𝘢𝘪𝘥𝘪𝘢 𝘬𝘶𝘪𝘮𝘢𝘳𝘪𝘴𝘩𝘢 𝘎𝘳𝘪𝘥𝘪 𝘺𝘢 𝘛𝘢𝘪𝘧𝘢, 𝘩𝘶𝘴𝘶𝘴𝘢𝘯 𝘸𝘢𝘬𝘢𝘵𝘪 𝘸𝘢 𝘩𝘪𝘵𝘪𝘭𝘢𝘧𝘶 𝘢𝘶 𝘤𝘩𝘢𝘯𝘨𝘢𝘮𝘰𝘵𝘰 𝘻𝘢 𝘶𝘱𝘢𝘵𝘪𝘬𝘢𝘯𝘢𝘫𝘪 𝘸𝘢 𝘶𝘮𝘦𝘮𝘦.

𝘔𝘧𝘶𝘮𝘰 𝘩𝘶𝘰 𝘶𝘮𝘦𝘶𝘯𝘨𝘢𝘯𝘪𝘴𝘩𝘸𝘢 𝘯𝘢 𝘣𝘦𝘵𝘳𝘪 𝘮𝘢𝘢𝘭𝘶𝘮 𝘻𝘪𝘯𝘢𝘻𝘰𝘸𝘦𝘻𝘦𝘴𝘩𝘢 𝘩𝘶𝘥𝘶𝘮𝘢 𝘺𝘢 𝘶𝘮𝘦𝘮𝘦 𝘬𝘶𝘦𝘯𝘥𝘦𝘭𝘦𝘢 𝘬𝘶𝘱𝘢𝘵𝘪𝘬𝘢𝘯𝘢 𝘩𝘢𝘵𝘢 𝘱𝘢𝘭𝘦 𝘨𝘳𝘪𝘥𝘪 𝘬𝘶𝘶 𝘪𝘯𝘢𝘱𝘰𝘬𝘢𝘵𝘪𝘬𝘢, 𝘩𝘢𝘵𝘶𝘢 𝘪𝘯𝘢𝘺𝘰𝘵𝘢𝘳𝘢𝘫𝘪𝘸𝘢 𝘬𝘶𝘰𝘯𝘨𝘦𝘻𝘢 𝘶𝘵𝘩𝘢𝘣𝘪𝘵𝘪 𝘯𝘢 𝘶𝘩𝘢𝘬𝘪𝘬𝘢 𝘸𝘢 𝘩𝘶𝘥𝘶𝘮𝘢 𝘺𝘢 𝘯𝘪𝘴𝘩𝘢𝘵𝘪 𝘬𝘢𝘵𝘪𝘬𝘢 𝘒𝘢𝘯𝘥𝘢 𝘺𝘢 𝘒𝘢𝘴𝘬𝘢𝘻𝘪𝘯𝘪.

𝘔𝘳𝘢𝘵𝘪𝘣𝘶 𝘸𝘢 𝘮𝘳𝘢𝘥𝘪 𝘩𝘶𝘰, 𝘔𝘩𝘢𝘯𝘥𝘪𝘴𝘪 𝘚𝘪𝘵𝘩𝘰𝘭𝘦 𝘔𝘸𝘢𝘬𝘢𝘵𝘢𝘨𝘦, 𝘢𝘮𝘦𝘴𝘦𝘮𝘢 𝘬𝘶𝘸𝘢 𝘶𝘵𝘦𝘬𝘦𝘭𝘦𝘻𝘢𝘫𝘪 𝘸𝘢 𝘮𝘳𝘢𝘥𝘪 𝘩𝘶𝘰 𝘶𝘵𝘢𝘪𝘮𝘢𝘳𝘪𝘴𝘩𝘢 𝘶𝘸𝘦𝘻𝘰 𝘸𝘢 𝘯𝘤𝘩𝘪 𝘬𝘢𝘵𝘪𝘬𝘢 𝘶𝘻𝘢𝘭𝘪𝘴𝘩𝘢𝘫𝘪 𝘯𝘢 𝘶𝘴𝘪𝘮𝘢𝘮𝘪𝘻𝘪 𝘸𝘢 𝘯𝘪𝘴𝘩𝘢𝘵𝘪 𝘫𝘢𝘥𝘪𝘥𝘪𝘧𝘶 𝘱𝘢𝘮𝘰𝘫𝘢 𝘯𝘢 𝘬𝘶𝘱𝘶𝘯𝘨𝘶𝘻𝘢 𝘶𝘵𝘦𝘨𝘦𝘮𝘦𝘻𝘪 𝘸𝘢 𝘶𝘮𝘦𝘮𝘦 𝘬𝘶𝘵𝘰𝘬𝘢 𝘒𝘦𝘯𝘺𝘢 𝘬𝘸𝘢 𝘢𝘫𝘪𝘭𝘪 𝘺𝘢 𝘶𝘴𝘢𝘸𝘢𝘻𝘪𝘴𝘩𝘢𝘫𝘪 𝘸𝘢 𝘷𝘰𝘭𝘵𝘢𝘨𝘦.

𝘈𝘪𝘥𝘩𝘢, 𝘬𝘪𝘵𝘶𝘰 𝘩𝘪𝘤𝘩𝘰 𝘬𝘪𝘵𝘢𝘬𝘶𝘸𝘢 𝘴𝘦𝘩𝘦𝘮𝘶 𝘮𝘶𝘩𝘪𝘮𝘶 𝘺𝘢 𝘮𝘢𝘧𝘶𝘯𝘻𝘰 𝘺𝘢 𝘷𝘪𝘵𝘦𝘯𝘥𝘰 𝘬𝘸𝘢 𝘸𝘢𝘯𝘢𝘧𝘶𝘯𝘻𝘪 𝘬𝘶𝘱𝘪𝘵𝘪𝘢 𝘮𝘧𝘶𝘮𝘰 𝘸𝘢 𝘍𝘢𝘤𝘵𝘰𝘳𝘺 𝘧𝘰𝘳 𝘛𝘦𝘢𝘤𝘩𝘪𝘯𝘨, 𝘢𝘮𝘣𝘢𝘰 𝘶𝘵𝘢𝘴𝘢𝘪𝘥𝘪𝘢 𝘬𝘶𝘬𝘶𝘻𝘢 𝘶𝘫𝘶𝘻𝘪 𝘸𝘢 𝘬𝘪𝘵𝘢𝘢𝘭𝘢𝘮𝘶 𝘯𝘢 𝘬𝘶𝘻𝘢𝘭𝘪𝘴𝘩𝘢 𝘸𝘢𝘵𝘢𝘢𝘭𝘢𝘮𝘶 𝘸𝘦𝘯𝘺𝘦 𝘶𝘸𝘦𝘻𝘰 𝘬𝘢𝘵𝘪𝘬𝘢 𝘴𝘦𝘬𝘵𝘢 𝘺𝘢 𝘯𝘪𝘴𝘩𝘢𝘵𝘪 𝘫𝘢𝘥𝘪𝘥𝘪𝘧𝘶 𝘯𝘤𝘩𝘪𝘯𝘪.

Ujenzi wa Jengo la Bweni katika Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI) 12/05/2026

Ujenzi wa Jengo la Bweni katika Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI)

Kampuni ya Chuo cha Ufundi Arusha ( ATC-PCB PLC) inaendelea na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Jengo la Bweni katika Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI) kwa kuzingatia viwango bora vya ubora, usalama na uimara wa miundombinu ya elimu.

Mradi huo unalenga kuboresha mazingira ya malazi kwa wanafunzi, kuongeza uwezo wa chuo kuhudumia idadi kubwa ya wanafunzi pamoja na kuimarisha mazingira rafiki ya kujifunzia na kuishi chuoni.

Katika utekelezaji wa kazi hiyo, ATC-PCB PLC imeendelea kutumia wataalamu wenye uzoefu, vifaa vya kisasa pamoja na usimamizi makini wa ujenzi ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

Ujenzi wa Jengo la Bweni katika Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI) Kampuni ya Chuo cha Ufundi Arusha (ATC-PCB PLC )inaendelea na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Jengo la Bweni katika Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI) kwa ...

11/05/2026

𝐔𝐣𝐞𝐧𝐳𝐢 𝐰𝐚 𝐊𝐢𝐰𝐚𝐧𝐝𝐚 𝐜𝐡𝐚 𝐌𝐚𝐟𝐮𝐧𝐳𝐨 𝐧𝐚 𝐔𝐳𝐚𝐥𝐢𝐬𝐡𝐚𝐣𝐢 𝐀𝐓𝐂 𝐖𝐚𝐬𝐡𝐢𝐤𝐚 𝐊𝐚𝐬𝐢

Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kinaendelea na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha Mafunzo na Uzalishaji wenye lengo la kuimarisha mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi pamoja na kuongeza uzalishaji wa bidhaa na huduma mbalimbali za kiufundi.

Mradi huo unatarajiwa kusaidia kukuza ubunifu, ujuzi wa kazi, na kuandaa wahitimu wenye uwezo wa kukidhi mahitaji ya soko la ajira na maendeleo ya viwanda nchini.

Kupitia kiwanda hicho, wanafunzi watapata fursa ya kujifunza kwa vitendo katika mazingira halisi ya kazi huku chuo kikiongeza mchango wake katika maendeleo ya teknolojia, utafiti na uchumi wa taifa.

𝐖𝐚𝐣𝐮𝐦𝐛𝐞 𝐰𝐚 𝐀𝐓𝐂-𝐏𝐂𝐁 𝐏𝐋𝐂 𝐰𝐚𝐭𝐞𝐦𝐛𝐞𝐥𝐞𝐚 𝐌𝐫𝐚𝐝𝐢 𝐰𝐚 𝐮𝐣𝐞𝐧𝐳𝐢 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐂𝐡𝐮𝐨 𝐜𝐡𝐚 𝐓𝐚𝐢𝐟𝐚 11/05/2026

https://youtu.be/NvcyipXajyE?si=bwesHXL9TMecbE2Z

ATC-PCB PLC ni kampuni ya ujenzi ya Chuo cha Ufundi Arusha inayojihusisha na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya miundombinu na majengo.

Kampuni inalenga kutoa huduma bora za ujenzi kwa kutumia wataalamu wenye uzoefu, teknolojia ya kisasa, na kuzingatia viwango vya ubora, usalama, na muda wa utekelezaji wa miradi.

Aidha, kampuni inachangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi kupitia ajira, mafunzo kwa vitendo, na ushirikiano na taasisi mbalimbali.

𝐖𝐚𝐣𝐮𝐦𝐛𝐞 𝐰𝐚 𝐀𝐓𝐂-𝐏𝐂𝐁 𝐏𝐋𝐂 𝐰𝐚𝐭𝐞𝐦𝐛𝐞𝐥𝐞𝐚 𝐌𝐫𝐚𝐝𝐢 𝐰𝐚 𝐮𝐣𝐞𝐧𝐳𝐢 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐂𝐡𝐮𝐨 𝐜𝐡𝐚 𝐓𝐚𝐢𝐟𝐚 ATC-PCB PLC ni kampuni ya ujenzi inayojihusisha na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya miundombinu na majengo. Kampuni inalenga kutoa huduma bora za ujenzi k...

Want your university to be the top-listed University in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address

P. O. Box 296
Arusha

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:00 - 15:00
Wednesday 07:00 - 15:30
Thursday 09:00 - 15:00
Friday 07:30 - 15:30