PDK generation
Tunashugulika na Kutoa Elimu ya Afya kwa ujumla. Deals with Health Education
Fuatilia Makala zetu YouTube kwa Channel yetu ya PDK Generation.
17/08/2025
JINSI YA KUGAWA FEDHA ZA BASKET FUND KWENYE MAKUNDI MBALIMBALI YA BIDHAA ZA AFYA
Asilimia 35 (35%) ya Fedha za Basket fund zinazoingia kwenye akaunti za benki za vituo vya kutolea huduma za afya zinatakiwa kutumika kwa ajili ya kununua bidhaa za Afya.
Hata hivyo, bidhaa za afya ziko katika makundi kadhaa, kwahiyo fedha hizo asilimia 35 zikishapatikana, zinatakiwa kugawanywa tena kwenye makundi ya bidhaa za afya k**a ifuatavyo:-
i) Dawa (Medicines) - 50%
ii) Vifaa tiba (Medical & Diagnostic equipments) - 15%
iii) Hospital supplies - 10%
iv) Vitendanishi vya maabara (Laboratory reagents) - 10%
v) Vifaa tiba vya huduma za Afya ya kinywa na meno (Dental equipments) - 10%
vi) Planned preventive maintenance (PPM) - 5%.
Kwa ufafanuzi zaidi na mfano, tazama makala hii YouTube ndani ya channel ya PDK Generation.
28/07/2025
JINSI YA KUPUNGUZA MADENI YA BIDHAA ZA AFYA BOHARI YA DAWA MEDICAL STORES DEPARTMENT MSD
Hali ya upatikanaji wa bidhaa za afya hapa Nchini imeendelea kuimarika siku hadi siku. Licha ya kuimarika huko, bado kuna changamoto kadhaa ambazo tunapaswa kukabiliana nazo. Mojawapo ya changamoto hizo ni madeni ambayo bohari ya dawa (medical stores department) inadai kwa baadhi ya wateja wake.
Madeni haya yana visababishi kadhaa ikiwemo matumizi ya fedha za mapato ya vituo yasiyofuata miongozo pamoja na kutoelewa vizuri kutafsiri taarifa mbalimbali zinazopatikana katika mifumo ya ugavi wa bidhaa za afya.
Katika makala hii kwenye YouTube channel ya PDK Generation tumeeleza kwa kutumia mifano halisi namna ambavyo makosa yanafanyika wakati wa kuagiza bidhaa za afya kwa waagizaji kushindwa kutafsiri vizuri taarifa zilizopo kwenye mfumo wanaotumia kuagiza unaofahamika k**a electronic logistics management information system (eLMIS)
15/06/2025
Clock Tower, Arusha Tanzania.
The midpoint between Cairo Egypt and Cape Town SA.
Exactly the centre of East Africa.
22/05/2025
JINSI YA KUJAZA REJESTA ZA KUTOLEA DAWA (DRUG DISPENSING REGISTERS)
Ili kufanya maamuzi sahihi kwenye sekta ya afya hasa kwenye eneo la bidhaa za afya, hatuna budi kuwa na takwimu sahihi ambazo ndizo hutengeneza taarifa za kufanyia maamuzi.
Moja ya nyenzo zinazotumika katika kuingiza taarifa za dawa ni rejesta za kutolea dawa (drug dispensing registers). Hizi zikijazwa vizuri na kwa usahihi tutapunguza changamoto nyingi katika eneo la dawa k**a vile dawa kuchina (expiries) na ukosefu wa dawa vituoni (Out of Stock - OS).
Katika makala hii ndani ya YouTube channel ya PDK GENERATION tumeeleza namna sahihi ya kujaza rejesta za kutolea dawa hasa katika eneo la kufanya majumuisho ambapo kwa kiasi kikubwa pana changamoto.
10/05/2025
MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WAFAMASIA TANZANIA PST ARUSHA 2025
Chama cha Wafamasia Tanzania - The Pharmaceutical Society of Tanzania (PST) kitafanya mkutano wake mkuu wa mwaka Jijini Arusha kuanzia tarehe 4 mpaka 6 mwezi juni mwaka 2025.
Mkutano huo utakua wa kipekee sana kwani mgeni rasmi atakua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Tazama video hii kwenye YouTube channel ya PDK Generation ili upate taarifa zaidi ikiwemo gharama za kushiriki.
09/05/2025
DAWA YA ASILI YA KUTIBU MAUMIVU YA PERIOD KWA WANAWAKE
Majani ya mti wa matunda aina ya mapera yameonekana kuwa na ufanisi mkubwa katika kutibu maumivu yatokanayo kwa wanawake, yale wanayoyapata kila mwezi "wanapoingia period" .
Utafiti uliofanywa kwa wanawake wanaokutana na maumivu hayo umeonesha kwamba majani hayo yanaweza kutumika k**a mbadala wa dawa zilizozoeleka k**a vile ibuprofen.
Tembelea YouTube channel ya PDK Generation upate kusikia mengi zaidi kuhusu mti huu.
26/04/2025
MTI SHAMBA UNAOWEKWA KWENYE POMBE YA ASILI YA ROMBO - MBEGE NI DAWA
Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) ambayo kwa miaka 12 imekua ikiufanyia utafiti mti dawa ambao unafahamika kwa jina la Mporojo au "Ormuktan" kwa kimasai, "mokuta" kwa kichaga na kisayansi k**a Albizia anthelmintica, imegundua kwamba mti huo una uwezo wa kuotesha nywele/kuzuia kipara.
Mmea huo umekua ukitumiwa na wamasai katika kutibu magonjwa mbalimbali k**a vile Malaria na Minyoo.
Kwa upande mwingine, magome ya mti huo yamekua yakitumika kwa miaka mingi na wakazi wa Rombo k**a moja ya viungo muhimu katika kutengeneza pombe yao ya asili inayojulikana k**a mbege.
Tembelea YouTube channel ya PDK Generation upate kusikia mengi zaidi kuhusu mti huu, na kuona magome yake yanayotumika kwenye Mbege.
17/04/2025
DAWA YA ASILI YA AJABU INAYOTIBU MINYOO NA ULEVI
Asilimia kubwa ya Dawa tunazotumia sasa, kihistoria zilitokana na mimea, na kabla ya teknolojia kukua kwa kiasi tunachoshuhudia sasa, dawa zilikua zinatumika za mitishamba zaidi.
Kwenye makala hii utaona moja ya mzizi ambao umekua ukitumika hapa kijijini kwa ajili ya kutibu changamoto mbalimbali za kiafya ikiwemo minyoo. Lakini kwengineko duniani, mzizi huu unatumika kutibu magonjwa mbalimbali pamoja na tatizo la Ulevi.
DAWA YA ASILI YA AJABU INAYOTIBU MINYOO NA ULEVI #dawa #asili #pombe DAWA YA ASILI YA AJABU INAYOTIBU MINYOO NA ULEVI Asilimia kubwa ya Dawa tunazotumia sasa, kihistoria zilitokana na mimea, na kabla ya teknolojia kukua kwa ki...
02/04/2025
Professor Mohamed Janabi Contesting for Regional Director of the World Health Organization WHO - Africa Region
The aspirant for the position of Director of the World Health Organization (WHO) Africa Region, Professor Mohamed Janabi, said he will make significant efforts to persuade all member countries of the organization in Africa to ensure they implement the Abuja Declaration.
Visit our YouTube channel - PDK Generation for more information on this.
01/04/2025
JINSI YA KUMTAMBUA MFAMASIA FEKI
Ufamasia ni moja ya fani zenye umuhimu mkubwa na inayohitajika katika maeneo mengi ndani na nje ya nchi kwenye sekta ya Afya. Ni kutokana na umuhimu wake mkubwa ndipo watu wachache wenye nia ovu hujipachika na kujifanya wao ni wafamasia wakati ukweli ni kwamba hawana taaluma hiyo ila tu wanajifanya kuwa wafamasia ili wapate maslahi yao binafsi.
Ni kutokana na changamoto hiyo na nyingine kadhaa, ikatengenezwa namna ambayo mtu yeyote kupitia tovuti ya baraza la Famasi Tanzania anaweza kuthibitisha k**a mtaalamu fulani ana uhalali au hana uhalali wa kufanya kazi k**a mfamasia Tanzania.
Sikiliza makala hii kwa umakini kupitia YouTube channel ya PDK Generation upate kujua namna ya kuthibitisha ufamasia wa mfamasia uliyemtilia mashaka.
21/03/2025
DAWA YA COLCHICINE INAYOTIBU MAGONJWA K**A GOUT , ARTHRITIS NA RHEUMATISM IKO KWENYE MMEA HUU
Mmea huu ambao kwa jina la kisayansi unajulikana k**a Gloriosa superba una kiasi kikubwa cha dawa ya colchicine ambayo hutumika katika kutibu na kuzuia ugonjwa wa gout (gauti) na magonjwa mengine kadhaa.
Mmea huu unaopatikana katika maeneo mbalimbali ya Bara la Africa na kwingineko duniani, kwa sasa upo hatarini kutoweka.
Ili kuuona mmea huu na kusikiliza mengi zaidi yanayouhusu, tembelea YouTube channel yetu ya PDK Generation.
06/03/2025
TANZANIA HEALTH SUMMIT THS PHARMACIST OF THE YEAR MFAMASIA WA MWAKA
Chukua dakika chache kumsikiliza Mfamasia wa mwaka 2024 Tanzania alivohojiwa na Taasisi ya Tanzania Health Summit (THS) Kazini kwake Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa.
Click here to claim your Sponsored Listing.