Carlos Ricky Wilson Kirimbai
Carlos R. W. Kirimbai is a Minister of the Gospel.
14/08/2026
12/08/2026
If you think knowledge is expensive, try ignorance.
K**a unadhani maarifa ni gharama, jaribu ujinga.
Nini shauku yako katika saa hii?
Je unahitaji Mungu na nguvu Zake?
Kwa kiasi gani matumizi ya muda wako na fedha zako unaakisi hii shauku ya saa unayodai unayo?
Kwa kiasi gani unawekeza katika kumjua Mungu kupitia kusoma kwako Neno, vitabu vya watumishi waliyopakwa mafuta na kufuatilia mahubiri na mafundisho yao?
Bibilia inazungumza kwa habari ya WANA WA ISAKARI, watu wenye akili ya kujua nyakati na kujua yale Israeli wanatakiwa kufanya.
Majira tuliyopo ni muhimu sana kukua katika kumjua Mungu kupitia Neno Lake na mafundisho, mahubiri na vitabu vya wapakwa mafuta ambao Mungu kawaleta maishani mwetu.
Hos 6:3 SUV
[3] Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua BWANA; kutokea kwake ni yakini k**a asubuhi; naye atatujilia k**a mvua, k**a mvua ya vuli iinyweshayo nchi.
Yn 17:3 SUV
[3] Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
Wekeza muda na mapato katika kujikuza katika kumjua Mungu maana ni rahisi sana kuhusiana na kumfuata Mungu.
Mungu alipoongea na Ibrahimu atoke kwenye nyumba ya baba yake, kwa jamaa zake na katika nchi yake hakumwambia aende wapi.
Alimwambia tu toka na akamuahidi kuwa atamwonyesha atakapokwenda.
K**a Ibarahimu alitaka kujua afakapokwenda ilibidi kwanza atii atoke.
Mungu aliendelea kumwongoza hatua kwa hatua.
Kutembea kwa imani haiwezekani k**a tusipojifunza kumtegemea na kumtumaini Mungu.
Mungu amesema kwenye Neno Lake kuwa atatufundisha na kutonyesha njia tutakayoiendea.
Ameahidi kutushauri huku jicho Lake likitutazama.
Mungu huwa hatoi ramani nzima.
Mungu anaongoza hatua inayofuata.
Neno Lake linasema kuwa hatua (na sio safari nzima) za mwenye haki zinathibitishwa na Bwana.
Mwamini Mungu katika hatua inayofuata anayokuongoza.
Ni muhimu kuwa na maono lakini k**a Mungu hajakuonyesha picha nzima usilazimishe maono bali mtumaini kila siku aziongoze hatua zako.
Ayubu alisema "Yeye aijua njia ninayoiendea..."
Ni wazi hapa kuwa Ayubu hakuwa anaijua njia ila alimwamini Yeye aijuaye njia.
Daudi akasema kuwa nyakati zake zipo mkononi mwa Mungu.
Japo hakuwa anajua itakuwaje lakini alimwamini Mungu aliyekuwa na nyakati Zake.
K**a nuru uliyo nayo inakuonyesha tu hatua inayofuata basi chukua hatua inayofuata hata k**a huelewi ni kwa nini inabidi uichukue.
Ukisubiri mpaka uoine picha nzima hutakaa uanze maana ukweli ni kwamba picha nzima ni kubwa mno kwa ajili yako kuibeba ndiyo maana Mungu anakuonyesha tu hatua inayofuata.
Ni maombi yangu na dua kuwa Mungu akaifunue njia Yake kwa ajili yako kwa kukuonyesha hatua inayofuata.
Click here to claim your Sponsored Listing.