Equip for Change

Equip for Change

Share

Equip for Change is a Not-for-Profit organization registered in Tanzania. We empower individuals& com

Photos from Equip for Change's post 08/06/2026

27/05/2026

Photos from Equip for Change's post 26/05/2026

“Mkopo si msaada — unahitaji mfumo, maono na nidhamu ili uwe chombo cha mafanikio na si chanzo cha madeni.”
Tunajenga jamii yenye watu wenye fikra sahihi, mifumo imara, na nidhamu ya mafanikio

19/05/2026

Equip for Change inasimama k**a daraja la matumaini na mabadiliko kwenye jamii. Kupitia mafunzo, msaada wa vitendea kazi na kampeni za uhamasishaji, tunawawezesha wajasiriamali wadogo, vijana na wanawake kujenga maisha bora na endelevu.

Tunajivunia kuwa sehemu ya safari ya kuwainua na kuwapa fursa ya kusimama imara, huku tukihimiza mshik**ano wa wadau wote katika kujenga taifa lenye usawa na maendeleo. Kila hatua tunayochukua ni uwekezaji katika mustakabali wa kizazi kijacho.

Photos from Equip for Change's post 15/05/2026

Leo tumesherehekea zaidi ya kuhitimu darasa — tumeshuhudia mwanzo wa safari mpya ya maisha yenye mwelekeo, nidhamu, na uhuru wa kifedha.

Hongereni sana Wahitimu 19 wa Financial Freedom Class 3 kwa kujitoa kwenu, uvumilivu, nidhamu, na moyo wa kujifunza. Mmeonyesha kuwa mafanikio ya kweli hayaanzi na pesa nyingi, bali huanza kwa kubadilisha FIKRA, kujenga MFUMO sahihi, na kuishi kwa NIDHAMU ya kila siku.

Katika safari hii mmejifunza: ✅ Kutengeneza na kusimamia bajeti
✅ Kujenga tabia ya akiba
✅ Kuwekeza kwa hekima
✅ Kusimamia madeni
✅ Kufuatilia matumizi ya fedha
✅ Kujenga urithi na maisha yenye kusudi

Mmekubali ukweli kwamba: 🔹 Mtazamo huamua maamuzi
🔹 Mfumo huamua mwelekeo
🔹 Nidhamu huamua matokeo
🔹 Kusudi huamua matumizi ya fedha
🔹 Mungu ndiye msingi wa hekima na mafanikio ya kweli

Tunaamini wahitimu hawa sasa ni mabalozi wa Uhuru wa Kifedha katika familia, makanisa, biashara, na jamii zao. Tunatarajia kuona maisha yaliyobadilika, maamuzi yenye hekima, biashara zinazokua, familia zenye amani ya kifedha, na viongozi watakaoleta mabadiliko chanya katika jamii.

📖 “Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu; bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji.” — Mithali 21:5

Safari ya kweli inaanza sasa.
Toka kwenye hustle kwenda kwenye freedom.
Toka kwenye matumizi yasiyo na mpango kwenda kwenye mfumo.
Toka kwenye hofu ya fedha kwenda kwenye amani na utawala.

Photos from Equip for Change's post 09/05/2026

Timu ya Equip for Change tukiendelea kujenga uwezo kwa wajasiriamali 100 wanaojiandaa kuomba mikopo ya 10% kutoka Halmashauri.

Katika mafunzo ya siku moja, washiriki walijifunza namna ya kuandaa “Maandiko ya Miradi” kwa kufuata mwongozo rasmi wa Halmashauri, pamoja na kujengwa katika NIDHAMU ya fedha ili kuishi kwa malengo, kulinda ndoto zao, na kuacha urithi wa mafanikio kwa vizazi vijavyo.

Tulisisitiza jambo moja muhimu:
“Mkopo si msaada — unahitaji mfumo, maono na nidhamu ili uwe chombo cha mafanikio na si chanzo cha madeni.”

Tunajenga jamii yenye watu wenye fikra sahihi, mifumo imara, na nidhamu ya mafanikio.

Photos from Equip for Change's post 08/05/2026

Equip for Change imeendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuinua jamii kupitia mafunzo na msaada wa vitendea kazi kwa wajasiriamali. Katika Kata ya Lugoba, taasisi hii imemkabidhi mama mmoja mashine ya kusaga viungo na lishe mbalimbali yenye thamani ya TZS 350,000, k**a sehemu ya kutambua juhudi zake baada ya kufanya vizuri kwenye mafunzo ya ujasiriamali.

Msaada huu si zawadi tu, bali ni nyenzo ya kumwezesha kuongeza thamani ya bidhaa zake na kupanua biashara, yake. Tukio hili linatoa mfano wa wazi wa jinsi elimu na msaada wa vitendea kazi vinavyoweza kubadilisha maisha ya mtu mmoja na kuleta mabadiliko chanya kwa jamii nzima.

Ni wito kwa wadau na jamii kushirikiana na Equip for Change katika kuendeleza jitihada hizi, ili wajasiriamali wengi zaidi wapate nafasi ya kusimama imara, kujitegemea, na kuchangia maendeleo ya taifa.

Photos from Equip for Change's post 07/05/2026

Katika maadhimisho ya Mbio za Mwenge, Halmashauri ya Kibaha DC ilizindua rasmi “Jukwaa la Vijana” tarehe 17 Aprili 2026, Mlandizi.

Want your organization to be the top-listed Non Profit Organization in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address

Box 80088
Arusha
255