Ulimwengu wa Michezo
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Ulimwengu wa Michezo, Public Figure, sinoni, Arusha.
https://www.instagram.com/shabanifundisports?igsh=MTZlcnBhNzhoNGJqZQ==
MICHEZO ZAIDI @YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB NA SIMBA SC TANZANIA
KARIBUNI SANA
hatufungamani na timu yoyote Ile usiache kunifollow kwa update zote
23/08/2026
Mechi ya jana nimefurahi sana uchezaji wa Geita gold Yani wanatandaza soka haswa
Kuna timu mbili zinaniogopesha tu kwa uhatari wake hii geita na tra united wanacheza Mpira mzuri sana
Naendelea kuzifatilia mechi zote kuona nani atakuwa wakushika Nafasi ya pili tatu na nne dhidi ya Simba SC Tanzania atalayeshika Nafasi ya pili
Azam FC simuoni kabisa kwenye kuwania Ubingwa kabisa
Young Africans Sports Club ni bingwa tena
Nafasi ya pili simba
Nafasi ya tatu itakuwa timu mgeni kabisa ✍️✍️✍️✍️
Ulimwengu wa Michezo
Shabani Fundi Sport
23/08/2026
Yani mpaka na msaada wa FVS bado jamaa katuongopea aiseeee 🤣
HAKUNA PENATI YA VILE MAISHA YOTE
23/08/2026
BUDO Aliyenenepa.
Siku ya kwanza kumuona tu nikasema atateseka sana hapa bongo
HUyo VICTOR SIMUONI hachambuliki sasa hv😅😅😅
23/08/2026
ALLY MNYUPE REFA AMBAYE ANATAKA KUCHUKUA NAFASI YA ABDALA KAMBUZI Kuwabeba KINYESI FC na kuharibu mechi za Young Africans Sports Club
Msimu uliopita alifungiwa dhidi ya Mechi ya Azm vs Yanga alikataa kabisa,pili akafungiwa mechi ya Kinyesi fc kwa kuwabeba.
Jana kawapa tuta lake la MOYONI licha FVS kuonyesha hakuna faulo MWAMBA KAFUNIKA tuta.
WALETENI SISI YANGA AFRICA tunaijua sana hiyo michezo.Nlishawaambia mkichezea Mambo ya kuharibu FOOTBALL Tanzania YANGA TUNAFANYA MARA 2 YENU MNAVYOFANYA🏃😅🏃
NB:Ila RED kadi Zitawaua😅😅
22/08/2026
PROPAGANDA MFUU HAZINA MASHIKO! 🔥
Ulimwengu wa Michezo
Ndugu zangu, unapoamua kuandaa propaganda yako, inatakiwa uwe umekamilika kweli. Ukitoa kitu, watu wajue hapa umeshusha kitu haswa! 😄
Hebu fikiria, Stephanie Aziz Ki amechelewa kujiunga na timu na ametambulishwa miongoni mwa wachezaji wa mwisho wa Young Africans Sports Club , halafu hapo hapo unataka aanze kwenye kikosi cha kwanza. Hivi ni kweli?
Kocha Manqoba Mngqithi anaelewa anachokifanya. Hawezi kuvunja mioyo ya wachezaji wengine, jambo ambalo Mwalimu hataki kulifanya. Anaijua timu yake, anajua uwezo na viwango vya kila mchezaji, na kila mmoja atapata nafasi kulingana na uwezo atakaoonyesha kwenye uwanja wa mazoezi.
Mimi naamini hata mchezaji mwenyewe, Aziz Ki, anajua hawezi kuja leo na kuanza kucheza moja kwa moja. Suala la kupata namba lina muda wake.
Stephanie ni mchezaji mkubwa, na Kocha Mngqithi anamjua vyema. Si alimuona kwenye ile mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya robo fainali dhidi ya Mamelodi Sundowns kule Afrika Kusini?
Suala ni muda tu ambao Aziz Ki atachukua nafasi yake. Kwa kile kikosi cha Yanga SC kilichopo sasa, hata ungepewa wewe nafasi ya kupanga kikosi, lazima uchanganyikiwe: nani aanze na nani akae benchi? 😂🔥
Alichokifanya Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, ni sawa na kukuletea vyakula vya aina zote halafu akakuambia chagua ule nini na nini uache. 🍽️😂
Kwa hiyo, kuendelea kumjadili Kocha Mngqithi na Stephanie Aziz Ki kwa presha zisizo na msingi ni kutaka kulivuruga benchi la ufundi pamoja na mipango yao.
K**a timu inapata matokeo, inashinda na kukusanya alama muhimu, hilo ndilo jambo la msingi kwa mashabiki na wanachama.
Watu wanataka MATOKEO, siyo nani amecheza! 💚💛🔥 Shabani Fundi Sport
22/08/2026
🔥⚽ SINGIDA BLACK STARS 🆚 SIMBA SC 🔥
Leo saa 12:00 jioni tunakutana kwenye mchezo unaoahidi burudani ya kiwango cha juu! 👀🔥
Ni mchezo wa mafundi wawili wa moto—Jeancy Mboma, kinda wa Singida Black Stars, dhidi ya Libasse Gueye wa Simba SC. 🇹🇿⚽
👊🏽 Vijana hawa wana uwezo wa kugeuza mchezo kwa muda wowote. Je, mmoja wao ataamua mechi leo? 👀🔥
⏰ Saa 12:00 Jioni
🏟️ Singida Black Stars 🆚 Simba SC Tanzania
Macho yote kwa mafundi! 🔥🔥
Mtoto wa kiume kabisa unajifanyia party ya birthday! Uko sawa au dirisha halina nondo? Wadogo zangu jifunzeni ku-focus na vitu vya kiume😡
21/08/2026
SHABIKI WA SIMBA ATANIA: “MAMA SAMIA, MTEUE RAIS WA YANGA KUWA BALOZI ILI TUPUMUE!”
Shabiki wa Simba SC Mzee Said, ametoa kauli ya kipekee kwa utani akisema angepata nafasi ya kukutana na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, angekuwa na ombi moja tu, kumteua Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said, kuwa Balozi katika nchi yoyote ile.
Kwa mujibu wa Mzee Said, sababu ya ombi hilo ni kuhakikisha Simba SC wanapata nafasi ya “kupumua kidogo” kutokana na namna ambavyo Yanga SC imekuwa ikiendeshwa kwa ufanisi chini ya uongozi wa Hersi.
Mzee Said amemsifu Kiongozi huyo kwa namna anavyosimamia klabu, hususan katika masuala ya usajili na uendeshaji wa timu kwa ujumla, akidai mafanikio ya Yanga SC katika kipindi cha sasa yameifanya klabu hiyo kuwa imara zaidi kiutawala na kisoka.
Kwa mtazamo wake, ubora huo wa uongozi ni miongoni mwa mambo yanayofanya Simba SC kupata wakati mgumu katika ushindani dhidi ya watani wao wa jadi.
Hivyo basi, Mzee Said anasema k**a angepata nafasi ya kumuona Mama Samia, angewasilisha ombi lake kwa mzaha lakini kwa msisitizo:
“Mama, mteue Haris kuwa Balozi, hata nchi yoyote ile, ili sisi Simba tupumue kidogo!”
Kauli hiyo imezua burudani kwa mashabiki wa soka kutokana na jinsi inavyodhihirisha ushindani mkali uliopo kati ya Simba SC na Yanga SC, ambao kila upande hutafuta mbinu ya kumzidi mwenzake.
Toa maoni yko Ulimwengu wa Michezo
21/08/2026
🔰🔰🔰SEKTA YA UANDISHI WA HABARI ilikuwa inaheshimika sana zamani lakini kadri siku zinavyoenda mbele sekta hii inazidi kupoteza heshima na nguvu yake. Hivi sasa mtu anajiamulia tu kujiita Mwandishi ilimradi ana uwezo wa kuuliza swali lolote, ilimradi anafanya kazi kwenye media fulani ama ana page mtandaoni.
Siku hizi mwandishi yupo radhi kudanganya watu kwa maslahi yake binafsi. Mbaya zaidi wanaodanganywa ni watu wanaomfuatilia siku zote pengine wanamuamini sana pia. Ubaya zaidi ni kwamba, waandishi hao uchwara wanatambua kuwa wanafuatiliwa na watu ambao hawana kawaida na hawapendi kufuatilia mambo kiundani yaani Chochote wanachopewa wanakipokea tu.🤔
Imagine, mtu anaamka asubuhi na kuamua kuandika uongo kwamba Selemani Mwalimu hachezi Young Africans Sports Club kisa Simba wamegoma kumuondoa kwenye mfumo wa FIFA connect. Watu hawajiulizi, inawezekanaje mchezaji wa Wydad akazuiliwe na Simba? Je na wengine wote ambao hawajacheza mfano Aziz Ki, Juma Abushiri, Mihambo nk nao wamezuiliwa?
Waandishi siku hizi wanapoteza weledi na hakika wasipobadilika na kuacha kutumika vibaya basi wataifanya kazi hii idharaulike sana...✍️
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the public figure
Telephone
Address
Arusha