Raphael Soingey

Raphael Soingey

Share

Founder | Enrich Generations Foundation
We provide Biblically-based, common-sense education and empowerment that gives HOPE to everyone in every walk of life.

Raising a generation of purpose. Transforming lives. Establishing Kingdom impact.

26/04/2026

Mungu anadai matunda kwako!

18/04/2026

Kitabu cha Mithali 17:22, kilinifanya nikumbuke Biology ya Form Two! Sikiliza kwa makini, na hutatunza tena uchungu moyoni mwako!

17/04/2026

“MAJIRA YA KUJILIWA KWAKO YATAKAPOTIMIA, NEEMA ITAKUTAFUTA POPOTE UTAKAPOKUWA”

Na Raphael Soingey

Kuna nyakati katika maisha ambapo kila kitu huonekana kuharibika.
Milango inafungwa. Watu muhimu huondoka. Mipango inavurugika.

Naomi alifika mahali hapo. Kitabu cha Ruthu

Aliondoka akiwa amejaa…
Akarudi akiwa mtupu.

Akasema: “Msiniite Naomi (yaani, mzuri), niiteni Mara (yaani, uchungu).”

Lakini hakujua jambo moja:

👉 Mungu alikuwa tayari ameweka mbegu ya urejesho ndani ya maisha ya Ruthu.

HOJA YA 1: HATIMA HUFICHWA KWENYE MAHUSIANO

Ruthu hakuwa Mwisraeli.
Hakuwa na agano, wala urithi, wala nafasi katika ardhi ya mji wa Bethlehem.

Lakini alifanya uamuzi wa ajabu:

«“Watu wako watakuwa watu wangu, na Mungu wako atakuwa Mungu wangu.”»

Alichagua uhusiano badala ya faraja.
Alichagua agano badala ya urahisi.

👉 Kuna mafanikio ambayo hayaji kwa maombi pekee—yanakuja kwa mpangilio sahihi wa mahusiano.

Kuna watu Mungu anakuunganisha nao:

- Sio kwa ajili ya starehe
- Sio kwa ajili ya urahisi
- Bali kwa ajili ya hatima yako

K**a Ruthu angebaki Moabu—angebaki wa kawaida.

Lakini kwa sababu alimfuata Naomi—
👉 Aliingia katika mpango wa Mungu.

HOJA YA 2: KONDENI SIYO MWISHO WAKO

Ruthu alipofika Bethlehem, hakuingia kwenye jumba la kifahari.
Aliingia kondeni.

Mahali pa:

- Kazi ngumu
- Unyenyekevu
- Kujificha

Alikuwa anaokota masazo ya nafaka.

Lakini sikia hili vizuri:

👉 Uliposimama sasa sio mwisho wa safari yako.

Kondeni ni mahali pa:
- Kupimwa tabia
- Kujengwa kiimani
- Kujifunza uaminifu

Wengi wanadharau kondeni( mwanzo wao mdogo).
Lakini kondeni ndiko mahali ambapo Boazi(Your destiny helper) atakuona.

HOJA YA 3: MIUNGANIKO YA KIMUNGU HAITOKEI K**A AJALI

Biblia haisemi Ruthu “alitokea tu” katika shamba la Boazi.

👉 Hakuna bahati katika hatima—kuna mpango wa Mungu.

Boazi alikuwa:

- Tajiri
- Mwenye heshima
- Mkombozi wa jamaa

Lakini Ruthu hakumkimbiza Boazi.

👉 Unapokuwa mtu sahihi, miunganisho sahihi itakutafuta.

HOJA YA 4: HESHIMA HUFUNGUA MILANGO KULIKO UPENDELEO

Boazi alisema:
“Nimesikia yote uliyomtendea Naomi.”

Ruthu alikuwa anaangaliwa—bila yeye binafsi kujua.

👉 Tabia yako ya siri ndiyo hujenga fursa zako za wazi.

Alikuwa:

- Mwaminifu bila kushangiliwa
- Mnyenyekevu bila kutambuliwa
- Thabiti bila kuonekana

Ghafla—neema ikaanza kunena!

HOJA YA 5: UKOMBOZI HUBADILISHA HADITHI YAKO

Boazi akawa mkombozi wa Ruthu.

Hakumsaidia tu—
👉 Alimbadilisha kabisa.

Kutoka:

- Mgeni → Familia
- Mjane → Mke
- Maskini → Mwenye nafasi

Hii ndio nguvu ya ukombozi.

Mungu haboreshi maisha yako tu—
👉 Anaandika upya historia yako.

HOJA YA 6: SAA YAKO IKITIMIA HADITHI YAKO ITABADILISHWA KABISA

Ruthu akamzaa Obedi
Obedi akamzaa Yese
Yese akamzaa Daudi

Mwanamke aliyekuwa mjane na mgeni…
👉 Akawa sehemu ya ukoo wa kifalme!

Sijui uko katika hatua gani sasa—
Labda uko kondeni(kwenye mwanzo wako duni):

Umechoka… umevunjika moyo… unajiuliza maswali mengi yasiyo na majibu …

Lakini sikia neno hili:

🔥 Mungu aliyemwona Ruthu—atakutambua na wewe pia
🔥 Mungu aliyemuunganisha Ruthu—atakuunganisha pia
🔥 Mungu aliyemrejesha Naomi—atakurejesha pia

👉 Hali yako ya sasa inakaribia kuwa mlango wako wa neema
👉 Mapambano yako yanakaribia kuwa ushuhuda wako
👉 Uaminifu wako unakaribia kuvuta hatima yako

---

HITIMISHO

Endelea kuwa mwaminifu
Endelea kuwa mnyenyekevu
Endelea kutii

Kwa maana wakati ukifika—

👉 neema itakufuata kondeni!

11/04/2026

Naomba usikilize hadi mwisho, naamini utajifunza kitu cha kukusaidia!
Ubarikiwe sana!

11/04/2026

SIRI YA MACHOZI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO
Machozi si udhaifu.
Machozi si kuchanganyikiwa.
Machozi ni lugha ya kiroho inayoeleweka kabisa mbinguni.
Kuna wakati katika maisha ambapo maneno hushindwa kutamkika kutokana na hali anayopitia mtu… lakini machozi yake huanza kunena!

1. Machozi ni maombi yasiyo na maneno
Wakati moyo umejaa kupita kiasi na huwezi kueleza, machozi yako huwa sauti yako mbele za Mungu.
“Nimesikia maombi yako; nimeyaona machozi yako.” — Isaya 38:5
Hii ina maana: Hata k**a huwezi kuomba vizuri…
Hata k**a uko kimya…
Machozi yako tayari yamesajiliwa mbinguni.

2. Machozi ni mbegu za furaha ya baadaye
Katika roho, hakuna kinachopotea—hata maumivu.
📖 “Wapandao kwa machozi watavuna kwa furaha.” — Zaburi 126:5
Kila tone la machozi unalolia kwa imani ni k**a mbegu ardhini.
Inaweza kuonekana k**a kupoteza leo, lakini kiroho:
•Maumivu yanapanda kusudi
•Mateso yanatengeneza ushuhuda
•Kulia kunajenga mavuno ya baadaye
Unacholia leo kinaweza kuwa unachosherehekea kesho.

3. Machozi huvuta umakini wa Mungu haraka kuliko maneno
Kuna maombi yanapanda polepole… lakini machozi hupanda kwa haraka.
📖 “Umehesabu machozi yangu na kuyaweka katika kiriba chako.” — Zaburi 56:8
Hii ina maana: Mungu hapuuzi maumivu ya moyo.
Kila tone la machozi linathaminiwa mbele zake.
Hakuna chozi unalolia kwa siri linalosahaulika mbinguni.

4. Machozi hutokea mahali ambapo nguvu za mwanadamu zinaishia
Machozi mara nyingi huja pale:
•Umefanya kila unachoweza
•Huna majibu tena
•Umeishiwa nguvu
Na hapo ndipo Mungu huanza kutenda.
Kwa maana mwanadamu anapoishia, Mungu huanza.

5. Si machozi yote ni maumivu—baadhi ni ushindi wa kiroho
Kuna machozi yanayokuja pale:
•Uponyaji unapoanza ndani yako
•Msamaha unapotolewa
•Mizigo inapopungua ghafla
•Amani inapoingia moyoni
Hayo si machozi ya huzuni…
Ni utoaji wa kiroho.

Kumbuka...
Ijapokuwa unalia sasa, haimaanishi Mungu amekuacha.
Inaweza kumaanisha:
•Mbingu iko karibu zaidi kuliko unavyofikiri
•Msimu mpya unaumbwa
•Kitu cha kiroho kinachakatwa kwa ajili ya ushindi wako
Kwa sababu kabla Mungu hajageuza maumivu kuwa furaha…
huruhusu machozi yafanye kazi yake.
Wakati mwingine maombi ya kina zaidi si yale yanayotoka kwenye maneno unayotamka…bali ni yale yanayokupelekea kutoa machozi zaidi.

K**a neno hili limekugusa, uwashirikishe na wengine wapate kutiwa moyo!

Ubarikiwe sana!

Raphael Soingey

11/04/2026

Mungu hachelewi kamwe—Yeye hufanya kila kitu kwa wakati wake

Kuna nyakati maisha yanakupeleka mahali ambapo maombi yanaonekana kutojibiwa kabisa. Unajihisi k**a vile Mungu amekufuta kwenye Kitabu chake cha Kumbukumbu. Unajihisi k**a Mungu hakumbuki tena k**a aliwahi kuumba kiumbe k**a wewe. Unaanza kuhisi k**a Mungu angekuja mapema, maumivu yasingekuwepo, na hasara isingetokea. Ndipo kimya cha moyo kinapouliza: “Mungu, uko wapi?”

Lakini hicho si kutokuamini—hicho ni roho iliyojeruhiwa ikitafuta maana ya kuchelewa kwa Mungu.

Katika kitabu cha Yohana Mtakatifu, sura ya 11, Lazaro alipougua, Yesu hakuharakisha kwenda kumhudumia. Alionekana kuwa mtulivu kana kwamba sio jambo la dharura. Wakati wengine wakidhani kuwa anachelewa kwenda kumhudumia rafiki yake aliyempenda, Yesu alikuwa akitembea kwenye ratiba ya mbinguni "divine timing." Alipoingia hatimaye, kaburi lilikuwa limekwisha kusema “mwisho.” Hata macho ya wanadamu yalikuwa yameshatoa hukumu.

Lakini Yesu hakuwahi kutazama kwa macho ya mwisho—Yeye hutazama kwa macho ya utukufu.
Ndiyo maana alisema: “Huu ugonjwa si wa mauti, bali kwa utukufu wa Mungu.”

Watu waliona kuchelewa kwa Mungu.
Yesu aliona maandalizi ya ufunuo mkubwa zaidi.
Kwa sababu kuna tofauti kati ya kile kilichokufa na kile kilichowekwa kwa ajili ya kufufuliwa.

Na aliposema: “Lazaro, njoo nje,” muda uliodhaniwa kuwa umefunga kila kitu ukapigwa na sauti ya uzima.

Hivyo elewa hili kwa kina:
Mungu akichelewa si kwa sababu hajali—ni kwa sababu anafanya kazi mahali macho yako hayaoni.
Kimya chake si kutokuwepo—ni ujenzi wa makusudi usioonekana.
Na kile unachoita “mwisho” mara nyingi ni mlango wa utukufu ambao haujafunguka bado.
Mungu hachelewi.

Yeye huingia pale ambapo mwanadamu amesema “imekwisha,” na kuandika “imeanza upya.”
Usikate tamaa. Historia yako bado iko mikononi mwa wakati sahihi wa Mungu.

10/04/2026

A man without purpose will always follow noise instead of direction.
Purpose gives you focus.
Without it, everything looks important.

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Arusha?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address

P. O BOX 14183
Arusha